Almasi Mswahili

Friday, 2 September 2016

TCU YATANGAZA UDAHILI AWAMU YA PILI

Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga
mfumo wa pamoja wa udahili tarehe 31/08/2016
saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji
waliofanikiwa kuomba udahili kwa mwaka wa
masomo 2016/2017.
Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa
kufanikiwa kutokana na sababu mbali mbali, Tume
inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya
pili kuanzia tarehe 12 hadi 23 Septemba 2016 ili
kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili.
1. Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi
kwenye awamu ya kwanza
2. Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa
kuomba katika awamu ya kwanza
3. Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao
walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao
kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,
4. Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya
“Cambridge” mwaka 2016 na matokeo yao
yameshatoka,
5. Waombaji waliofaulu mitihani ya RPL,
6. Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao
kuwa na uthibitisho toka vyuo vyao vya awali.
Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili
kuruhusu taratibu zingine za kiudahili kuendelea
kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na vyuoni.
Asanteni
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
02 Septemba 2016

No comments:

Post a Comment