Almasi Mswahili

Tuesday, 6 September 2016

ONYO KWA WASIMAMIZI MTIHANI WA DARASA LA SABA

  Na Almasi Mswahili
Ikiwa yamesalia masaa kadhaa kabla ya kuanza kwa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi hapo kesho na kesho kutwa (Jumatano tarehe 7/9/2016 na Al-hamis tarehe 8/9/2016)
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Ileje Haji Mnasi, amewaasa wasimamizi wa mitihani
ya kumaliza elimu ya msingi kutofanya kazi kwa
mazoea ili kutoruhusu mianya itakayowafanya
wanafunzi wasiokuwa na uelewa kufaulu mitihani
hiyo.
Alisema kumekuwa na baadhi ya wanafunzi
wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu mithani
hiyo kitendo kinachotia mashaka kwa wasimamizi
hao kushindwa kunyakazi waliyopewa kwa makini.
Mnasi aliyasema hayo jana, wakati akitoa semina
ya mafunzo kwa wasimamizi wa halmashauri ya
wilaya ya Ileje ambapo alisema usimamizi hafifu wa
mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi
wasiokuwa na uwezo kitaaluma.
Aidha kabla ya uteuzi wa Rais wa jamhuri ya
muungazo wa tanzania Dr John Pombe Magufuli
mkurugenzi huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu
alikuwa afisa elimu shule ya msingi manispaa ya
iringa alisema iwapo ikibainika kufaulu kwa
wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika mtuhumiwa
wa kwanza kwenye uzembe huo atakuwa msimamizi
wa mitihani na hatua kali zitachukuliwa zidi yake.
“Nawatahadharisha kwamba mnaweza mkarubuniwa
kuwawezesha wanafunzi wasiokuwa na sifa wafaulu
mitihani hiyo,kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za
usimamizi na uendeshaji wa mtihani na kuwaambia
hayupo tayari kutumbuliwa na rais kwasababu za
wasimamizi”alisisitiza Mnasi.
Hata hivyo Mnasi aliwataka wasimamizi hao kuwa
makini katika kufanyakazi hiyo na kama kuna
jambo lolote ambalo hawajalielewa kuhusu kazi hiyo
ni vyema wakauliza ili kupewa majibu.
“hakikisheni kuwa taratibu zote za mitihani
zinazingatiwa ipasavyo na kuwataka wasimamizi
wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa
hali ya juu.“Nawaasa wasimamizi wa mitihani
kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani
serikali itachukua hatua kali kwa yeyote
atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani,”
alisema Mnasi.
Mnasi alibainisha kuwa, serikali imezingatia uwezo
wa kitaaluma, uadilifu na uaminifu hivyo
wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia
mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.
Aliongeza kuwa mitihani hiyo ni muhimu ili
kuliwezesha taifa kupima kiwango cha elimu
kilichpo nchini na kuwapata wasomi wa kiwango cha
juu.
Nao wasimamizi wa mitihani hiyo wamemuahidi
mkurugenzi huyo kuwa watasimamia mitihani hiyo
kwa kufuata sheria na kanuni za usimamizi wa
mitihani walizopewa.

No comments:

Post a Comment