MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilayani Urambo
mkoani Tabora, imemuhukumu Deus Barnaba(45)
kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkuta na
hatia ya kumnajisi mwanafunzi wa darasa la tatu
mwenye umri wa miaka tisa.
Akitoa hukumu hiyo mwishoni wa wiki iliyopita,
Hakimu Mkazi, Baptista Kashusha, alisema
mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na
upande wa mashitaka hivyo kumuona mshitakiwa
ana hatia.
Alisema adhabu hiyo iwe fundisho kwa watu
wengine wenye nia ya kufanya vitendo hivyo.
Hakimu Kashusha alisema mashahidi nane
walioletwa mahakamani hapo walithibitisha kuwa
mshitakiwa alitenda kosa hilo.
Mashahidi hao ni pamoja na daktari aliyempokea
mlalamikaji na kutoa fomu namba tatu (PF3)
iliyoonesha kuwa binti huyo aliumizwa katika
sehemu za siri.
Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, ,Joseph
Mbwana, alieleza mahakama hiyo kuwa Machi 27,
mwaka huu, majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji
cha Mwangaza wilayani Urambo, Deus alimnajisi
binti mwenye umri wa miaka tisa na kumsababishia
maumivu makali katika sehemu zake za siri.
Aidha, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa
mshitakiwa ili kukomesha matendo ya ubakaji
kabisa kwani mtuhumuwa anaonekana ni mtu
mwenye akili timamu, alifanya hivyo kwa makusudi
tu.
Hata hivyo, mshitakiwa huyo aliiomba mahakama
impunguzie adhabu kwakuwa ni mkosaji wa mara ya
kwanza na ana wazazi, mke na watoto
wanaomtegemea.
Welcome to our blog,this blog is deals with the all news about education and it allow teachers and other education dealers to discuss different things.
Sunday, 21 August 2016
AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA MIAKA 9
Labels:
Mswahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment