WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia
na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako amesema hadi sasa wizara
hiyo haina deni inayodaiwa na walimu
nchini na kwamba madeni yaliyokuwepo
ya Sh bilioni 22 yalishalipwa.
Profesa Ndalichako alisema hayo juzi
jioni wakati akizungumza kwenye
kipindi cha Tunatekeleza
kinachorushwa hewani moja kwa moja
na Kituo cha Televisheni cha Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC1).
Akizungumzia madeni ya walimu,
alisema serikali inawajali walimu
nchini na zipo jitihada mbalimbali
zimekuwa zikifanywa kuhakikisha madai
yao yanahakikiwa na kulipwa ili
kuepuka malimbikizo.
Alisema madeni ya walimu yako ya
aina mbili; moja ni madeni ya
mishahara ambayo wao wizara
hawayashughulikii bali yapo chini ya
Ofisi ya Rais, Utumishi na kwamba
madai aina ya pili ni yale yasiyo na
mshahara kama vile likizo, matibabu
na mengineyo, ambayo yako chini ya
wizara yake na hadi sasa wameshalipa
Sh bilioni 22 na hakuna madeni
mengine kutoka kwa walimu na
kuwataka walimu nchini kama wana
madeni mapya kuanzia sasa
wayawasilishe wizarani kwa ajili ya
kuhakikiwa na kulipwa.
“Wizara tunatambua mchango wa walimu
na umuhimu wao kwa upande wetu,
hatuna madai yoyote ya walimu yale
yanayotuhusu, kwa sababu huwa tuna
utaratibu wa kulipa kadri
tunavyoyapata na kama yapo kwa sasa
wayalete, fedha za kulipa zipo,”
alisema Profesa Ndalichako.
Akizungumzia suala la watumishi
hewa, Profesa Ndalichako alisema ni
vyema walioguswa katika uhakiki huo
unaoendelea kufanywa na timu ya
watendaji kutoka taasisi mbalimbali,
wakiwemo wakurugenzi, wakajiondoa
wenyewe kwenye ajira kwa sababu
mashtaka yanawangoja.
Kuhusu uhakiki wa wanafunzi wa elimu
ya juu, Profesa Ndalichako alisema
hadi sasa wamekamilisha uhakiki wa
vyuo 31 kati ya vyuo 80 vilivyopo
nchini na wameshabaini wanafunzi hewa
2,921 ambao hawakujitokeza wakati wa
uhakiki, licha ya matangazo na
msisitizo kutolewa.
Profesa Ndalichako alisema wakati
kazi ya uhakiki ilipoanza, walitoa
matangazo katika vyuo vyote na pia
vyuo navyo vilitoa matangazo kwenye
mbao za matangazo vyuoni na pia
kupitia vyombo vya habari na pia
kupitia serikali ya wanafunzi katika
vyuo husika, lakini idadi hiyo
haikujitokeza kuhakikiwa.
Alisema kwa wale wachache waliopuuza
kuhakikiwa hata kama wako mwaka wa
mwisho wa masomo, bado watatambulika
kama wanafunzi hewa hadi pale
watakapohakikiwa na hiyo itawagharimu
kulipa gharama za kufanyiwa uhakiki
huo.
Akizungumzia changamoto za wanafunzi
kutojua kusoma na kuandika, Profesa
Ndalichako alisema serikali imekuwa
imetoa mafunzo kwa walimu
wanaofundisha darasa la kwanza na la
pili na kwamba kadri muda
unavyosonga ndivyo tatizo
linavyoondoka.
Kuhusu utaratibu wa utoaji mikopo
kwa elimu ya juu, Profesa Ndalichako
alisema changamoto zipo kutokana na
mfumo uliokuwa ukitumika, lakini
hatua zimeshaanza kuchukuliwa ili
kuuboresha ili kuhifadhi kumbukumbu
za wanufaika ili iwe rahisi kuzidai.
Aidha, alisisitiza wanafunzi
waliomaliza shahada zao katika vyuo
mbalimbali nchini na ikagundulika
kuwa walizipata kwa njia ya rushwa,
ikibainika watanyang’anywa.
Chanzo: Habari Leo.
Welcome to our blog,this blog is deals with the all news about education and it allow teachers and other education dealers to discuss different things.
Saturday, 10 September 2016
WAZIRI:TUMESHAMALIZANA NA WALIMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment