MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilayani Urambo
mkoani Tabora, imemuhukumu Deus Barnaba(45)
kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkuta na
hatia ya kumnajisi mwanafunzi wa darasa la tatu
mwenye umri wa miaka tisa.
Akitoa hukumu hiyo mwishoni wa wiki iliyopita,
Hakimu Mkazi, Baptista Kashusha, alisema
mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na
upande wa mashitaka hivyo kumuona mshitakiwa
ana hatia.
Alisema adhabu hiyo iwe fundisho kwa watu
wengine wenye nia ya kufanya vitendo hivyo.
Hakimu Kashusha alisema mashahidi nane
walioletwa mahakamani hapo walithibitisha kuwa
mshitakiwa alitenda kosa hilo.
Mashahidi hao ni pamoja na daktari aliyempokea
mlalamikaji na kutoa fomu namba tatu (PF3)
iliyoonesha kuwa binti huyo aliumizwa katika
sehemu za siri.
Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, ,Joseph
Mbwana, alieleza mahakama hiyo kuwa Machi 27,
mwaka huu, majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji
cha Mwangaza wilayani Urambo, Deus alimnajisi
binti mwenye umri wa miaka tisa na kumsababishia
maumivu makali katika sehemu zake za siri.
Aidha, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa
mshitakiwa ili kukomesha matendo ya ubakaji
kabisa kwani mtuhumuwa anaonekana ni mtu
mwenye akili timamu, alifanya hivyo kwa makusudi
tu.
Hata hivyo, mshitakiwa huyo aliiomba mahakama
impunguzie adhabu kwakuwa ni mkosaji wa mara ya
kwanza na ana wazazi, mke na watoto
wanaomtegemea.
Welcome to our blog,this blog is deals with the all news about education and it allow teachers and other education dealers to discuss different things.
Sunday, 21 August 2016
AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA MIAKA 9
WATUMISHI HEWA WAONGEZEKA
Taarifa rasmi ya mwisho ya utekelezaji wa zoezi la
kuwaondoa watumishi hewa serikalini na taasisi
zake zote, itawasilishwa kwa Rais John Magufuli
Ijumaa wiki ijayo.
Hadi sasa
wameshabainika watumishi hewa 16,127 na
wameondolewa kwenye mfumo wa utumishi.
Aidha, mbali ya serikali kuokoa Sh bilioni 16.15
kwa mwezi huu wa Agosti baada ya watumishi hewa
hao kuondolewa kwenye mfumo wa utumishi, ambao
kama wasingeondolewa fedha hizo zilikuwa ziwalipe
mshahara, posho na malipo mengine, waajiri 145
hawajawasilisha taarifa kuhusu uhakiki wao.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora,Mh. Angella Kairuki alipozungumza na
waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam
kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la
kuwataka waajiri wote wa umma na serikali,
kuwaondoa watumishi hewa.
Akifafanua taarifa hiyo, Kairuki alisema Agosti
26, mwaka huu watamkabidhi rais taarifa rasmi ya
utekelezaji wa agizo hilo huku akiwataka waajiri
145 ambao hawajawasilisha taarifa za ama uwepo
wa watumishi hewa au la, kuhakikisha
wanaziwasilisha taarifa hizo kabla ya Ijumaa wiki
ijayo.
“Tunawapa muda hadi Ijumaa wiki ijayo wawe
wamewasilisha taarifa za kama wana watumishi
hewa au la na sisi Agosti 26, mwaka huu ndio
tunamkabidhi rais taarifa rasmi ya mwisho ya
utekelezaji wa agizo alilotoa,” alisema Kairuki
akizungumzia hatua ya Rais Magufuli kuagiza
uhakiki huo Machi mwaka huu.
Akielezea hatua zilizochukuliwa hadi sasa na waajiri
hao, Kairuki alisema nchi ina jumla ya waajiri 409
wa serikali na taasisi mbalimbali za umma, na kati
ya waajiri hao, hadi sasa waajiri 264 ndio
waliowasilisha taarifa za utekelezaji wa agizo hilo.
Alisema kati ya waajiri hao 264 waliowasilisha,
waajiri 63 wamethibitisha hawana watumishi hewa,
huku waajiri 201 wakibaini uwepo wa watumishi
hewa kuanzia mmoja na kuendelea.
“Tumepokea taarifa za utekelezaji wa agizo la rais
alilitoa Machi 15, mwaka huu na hadi sasa waajiri
264 kati waliotekeleza agizo hilo, 201 wamebaini
wana watumishi hewa,”
alisema Kairuki.
Akizungumzia hatua zitakazochukuliwa baada ya
kufikia tarehe ya mwisho wa kupeleka taarifa hizo,
Kairuki alisema jukumu lao ni kuzipokea na
kukabidhi mamlaka ya uteuzi ambayo ndiyo iliagiza
na ambayo ndiyo itaamua hatua za kuchukua.
Sambamba na hilo, Kairuki alisema hadi sasa jumla
ya watumishi hewa 606, wameanza kuchukuliwa
hatua za kisheria, ikiwemo mashauri yao kupelekwa
polisi na hivi sasa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia
Rushwa (Takukuru), wanafanya uchunguzi na
hatimaye watuhumiwa hao wafikishwe kwenye
vyombo vya juu vya sheria.
Aidha, maofisa utumishi 233 waliohusika kwenye
malipo ya mishahara hewa mashauri yao,
wamefikishwa kwenye mamlaka husika kwa
uchunguzi, ilhali watatu wamefukuzwa kazi, huku
wizara ikiendelea kufanya uchunguzi kwenye taasisi
75 za umma ili kujiridhisha kuhusu suala la
watumishi hewa.
Kuhusu waajiri 145 ambao hawajawasilisha taarifa
za uhakiki wa watumishi wao, Kairuki alisema zimo
taasisi, wakala, bodi, mabaraza, vyuo, hospitali,
ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa, tume na
mamlaka kadhaa ambazo hazijawasilisha taarifa
zao.
Kwa upande wa mabaraza nchini, Kairuki alisema
mabaraza mbalimbali 10 hayajawasilisha taarifa za
uhakiki wa watumishi na baadhi yao ni kama vile
Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), Baraza la
Elimu ya Ufundi (Nacte), Baraza la Taifa la
Biashara (TNBC), Baraza la Mitihani la Taifa
(NECTA) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Aidha, jumla ya vyuo vya umma 25 nchini
havijawasilisha taarifa zao za uhakiki wa watumishi
hewa na baadhi yao ni Dodoma (Udom), Chuo
KIkuu Huria (OUT), Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS), Chuo cha Diplomasia, Chuo Kikuu cha
Elimu Dar es Salaam (Duce), Chuo cha Usimamizi
wa Fedha (IFM) na Chuo cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere na Chuo Cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT).
Upande wa Bodi mbalimbali ambazo hazijawasilisha
taarifa zao jumla yake ni 10 na baadhi ya bodi hizo
ni pamoja na Bodi ya Korosho Tanzania, Bodi ya
Tumbaku, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu
ya Juu (HESLB) na Bodi ya Utalii na Bodi ya
Maziwa.
Pia zimo hospitali teule za rufaa tatu ambazo ni
Hospitali ya CCBRT, Hospitali ya Rufaa Bugando
na Hospitali ya Rufaa KCMC na kwamba katika
hospitali kama hizo zilizowasilisha taarifa zake,
wamebainika na kuondolewa watumishi hewa 4,000.
Kwenye taasisi za Umma na Wakala ambazo
hazijawasilisha taarifa zao jumla ziko 30 na baadhi
yao ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mfuko
wa Pembejeo za Kilimo, Makumbusho ya Taifa,
Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Shirika la
Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Madini la Taifa
(Stamico), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI),
Wakala wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na
Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).
Pia zipo Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa 12
ambazo baadhi yake ni Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa
wa Arusha, Dodoma, Dar es Salam, Mbeya, Pwani
na Kagera; kwa upande wa mamlaka zipo sita
ambazo ni Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),
Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa
Mauzo ya Nje (EPZA), Mamlaka ya Udhibiti wa
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu (CDA).
Aidha, zipo tume 10 ambazo hazijawasilisha taarifa
zake na baadhi yake ni Tume ya Pamoja ya Fedha,
Tume ya Atomiki, Tume ya Elimu Taifa, Tume ya
Kudhibiti Dawa za Kulevya, Tume ya Sayansi na
Teknolojia Tanzania na Tume ya Vyuo Vikuu
Tanzania (TCU).
Pia zipo Mamlaka za Serikali za Mitaa 38 zikiwemo
Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Manispaa ya Iringa,
Nyamagana, Halmashauri ya Mji, Kasulu,
Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma na Halmashauri
ya Wilaya ya Misenyi.
Wednesday, 17 August 2016
WAZIRI WA ELIMU ATOA WIKI MOJA VYUO VIREJESHE FEDHA
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Prof. Joyce Ndalichako ametoa siku saba kwa vyuo vikuu vilivyopokea fedha za wanafunzi ambao hawapo vyuoni kwa mwaka wa 2015/16 kuzirejesha wizarani mara moja.
Taarifa hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam mbele ya maafisa kutoka wizarani mwake,pamoja na kaimu mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo.
Thursday, 11 August 2016
FAIDA 13 ZA KULA PILIPILI
1.Kutibu kidonda-Hii inaweza kuwa ni ajabu kwa walio wengi lakini ni tiba liyothibitishwa na imekuwa ikitumika miaka kadhaa iliyopita katika nchi mbalimbali.Sio tu kuzuia kutokwa na damu katika kidonda cha kujikata kama ilivyozoea kutumiwa na wengi huko majumbani kwa miaka mingi bali pia huzuia fangasi na bakteria kuingia katika uwazi wa kidonda hicho hutumika pia kuondoa sumu mwilini
2.Hufanya mwili kuweza kutumia vyema virutubisho vipatikanavyo kutokana na chakula
3.Husaidia uyeyushaji wa mafuta mwilini/Kuchoma mafuta
4.Pilipili ina antioxidants muhimu kama beta carotene,ina wingi wa vitamini A,C na K hebu tuziangalie vitamini hizo:
(i)Vitamini A husaidia kuweka sawa kinga ya mwili pia hutukinga na kansa na magonjwa ya moyo
(ii) Kazi ya vitamini C-ni kuzuia Stroke,magonjwa ya moyo,macho na kansa mbalimbali.Miili ya binadamu haiwezi kujitengenezea vitamini C,hivyo basi tunaweza kupata vitamini C kupitia chakula.
(iii) Vitamini K-Husaidia katika ukuwaji wa mifupa,pia ni muhimu katika mzunguko wa damu.Pilipili zote huwa na Capsaicin ambayo kazi yake ni kupunguza maumivu,kuzuia kansa na magonjwa ya moyo.
5.Inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu
6.Huwasaidia watu wanene(over weight) au wanaougua ugonjwa wa kisukari.Hii ni kwa mujibu wa watafiti katika chuo kikuu cha Tasmania uliochapishwa katika American Joarnal of Clinical Neutition mwezi julai 2006.
7.Inasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa INSULIN kwa 60% baada ya kula chakula
8.Husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa RHEMATOID na ARTHRITIS kupata nafuu
9.Husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja mwilini
10.Husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua na kukufanya upumue kwa urahisi.
11.Husaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya utumbo.
12.Husaidia kuongezeka kwa kiwango cha METABOLIC kwa 23% ndani ya masaa matatu baada ya kuitumia. Hii pia husaidia kuchoma mafuta katika mwili.
13.Husaidia kupunguza cholestro na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.